Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo leo Oktoba 1,2024.
Mhe. Chana amefanya kikao na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Msalika Makungu, Mkuu wa Wilaya Sumbawanga, Nyakia Chirukile na baadhi ya Maafisa ya Waandamizi wa Mkoa wa Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa kuelimisha wananchi kuacha kuanzisha moto kwenye misitu, kupanda miti pamoja na kuainisha maeneo ya wananchi yenye changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa ajili ya kuwavuna.
Aidha, Mhe. Chana amesema changamoto zote zinazoihusu sekta ya Maliasili na Utalii zitafanyiwa kazi huku akisisitiza wananchi wanaojishughulisha na shughuli za ufugaji nyuki ni lazima wapewe elimu ya kutumia mizinga ya kisasa ili waweze kuzalisha asali kwa kiwango kikubwa.