BIDHAA ZA TANZANIA ZAVUTIA WENGI MAONESHO YA JUA KALI SUDAN KUSINI


Na: Mwandishi Wetu – Juba, Sudan Kusini

Bidhaa za Tanzania katika maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali zimekuwa kivutio kwa watu mbalimbali waliotembelea Banda la Tanzania kwenye Viwanja vya Freedom Hall, Juba Sudan ya Kusini.

Aidha, Bidhaa hizo ni pamoja na vikapu, pochi za wanawake, nafaka, tiba za asili, mvinyo (wine), viungo vya chakula, batiki, bidhaa za Ngozi, asali, urembo, samani (viti, meza).

Wakizungumza Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania wamesema maonesho hayo ya 24 ya Nguvu Kazi au Jua Kali yamewapatia fursa ya kutangaza bidhaa zao sambamba na kukuza masoko ya bidhaa zao na huduma wanazotoa.

Kwa upande mwengine, Wananchi wa Sudan ya Kusini wameonyesha kuvutiwa na bidhaa za wajasiriamali wa Tanzania na kueleza kuwa bidhaa hizo zina ubora na ujuzi wa hali ya juu.

Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanaongozwa na kauli mbiu “Kukuza Ubunifu wa Kipekee na Maendeleo ya Ujuzi miongoni mwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post