Uongozi wa Wasafi Media Unasikitika Kutangaza Kifo Cha aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi Cha Mashamsham cha Wasafi FM Khadija Shaibu ( Maarufu kama Dida).
Dida atakumbukwa kwa Uhodari wake na Ubora wake Kwenye Tasnia ya Habari, Uliompelekea Kuwa Mtangazaji Namba Moja wa Kike Nchini na Kuwa Kioo kwa Wanawake na Watangazaji Wengi waliokuwa wanamtazama kama Mfano.
Tunaungana na Ndugu , Jamaa na Marafiki Wote Kusheherekea Maisha Ya DIDA , Na Kuenzi Yale Mengi Mazuri aliyoyafanya Kwenye Jamii na tasnia ya Uandishi wa habari .
Tunamuombea Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi , Amen .
#KwaheriMalkiaWaKipaza #TutaonanaBaadae
Social Plugin