Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 kimefanyika leo, Oktoba 14, 2024, katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Kiongozi wa Mbio za mwaka huu 2024, Godfrey Mzava.
Mbio hizi pia zimeambatana na kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Tukio hilo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, ambayo imeanza Oktoba 8, 2024, na ilijumuisha shughuli mbalimbali kama kongamano la fursa za ujasiriamali kwa vijana na maonyesho ya bunifu za vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Social Plugin