Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PPRA YATOA MAFUNZO YA UNUNUZI WA UMMA KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA, WAKILI MTATIRO ATAKA YASAIDIE KULETA UWAZI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua Mafunzo  kuhusu Manunuzi ya Umma kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na PPRA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katika juhudi za kuimarisha uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imetoa mafunzo muhimu kuhusu Ununuzi wa umma kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwajengea waandishi uelewa wa kina kuhusu mifumo, taratibu, na sheria zinazohusiana na ununuzi wa umma.

Miongoni mwa mifumo hiyo ni pamoja na Mfumo wa NeST (National e-Procurement System of Tanzania) unaosaidia katika njia mbalimbali hasa katika mchakato wa ununuzi wa umma.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na PPRA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano, Oktoba 23, 2024. 

Wakili Mtatiro amesisitiza kwamba waandishi wa habari wana jukumu kubwa katika kusimamia uwajibikaji na kuwajulisha wananchi kuhusu matumizi ya rasilimali za umma.

 “Uelewa wa masuala ya manunuzi ni muhimu kwa maendeleo ya jamii zetu. Mnaweza kuwa daraja kati ya serikali na wananchi katika kuhakikisha uwazi,” amesema.

Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus amesema ni muhimu kwa waandishi kuelewa kanuni za ununuzi wa umma ili waweze kutoa habari sahihi na za kuaminika.

“Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya PPRA na waandishi wa habari. Tunatarajia waandishi watatumia maarifa haya katika kuandika habari zinazohusiana na ununuzi wa umma na kusaidia kuleta uwazi,” amesema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Patrick Mabula, amesema mafunzo hayo yameimarisha uelewa wa waandishi wa habari na kuwasaidia katika kutimiza wajibu wao wa kutoa taarifa sahihi na za kuaminika kwa jamii.

Mafunzo haya yanatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika uandishi wa habari na kuongeza uelewa wa masuala ya manunuzi ya umma miongoni mwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua Mafunzo  kuhusu Manunuzi ya Umma kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na PPRA. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua Mafunzo  kuhusu Manunuzi ya Umma kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na PPRA
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua Mafunzo  kuhusu Manunuzi ya Umma kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na PPRA
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula akitoa taarifa kuhusu mafunzo hayo
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com