Ulikuwa ni usiku wa shangwe na furaha wa tasnia ya Habari Nchini kwa kushuhudia Mwandishi mahiri na kiongozi kwenye sekta ya habari Bwana Edwin Soko aliposhiriki sherehe ya kuagwa kwa mchumba wake (Mke mtarajiwa) Lulu Samson Mbwaga.
Sherehe hiyo imefanyika tarehe 29/10/2024 katika ukumbi wa Landmark, Tukuyu Jijini Mbeya na kuhudhuria na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo waandishi wa habari toka Mikoa mbalimbali, viongozi wa dini, ndugu jamaa na marafiki kutoka familia ya Chrisantus Soko na Samson Mbwaga.
Usiku huo ulijawa na furaha na hisia mbalimbali, ambapo Edwin, mwandishi wa habari maarufu, akiwa na wapambe wake kutoka Mwanza na maeneo mengine walihudhuria kwa wingi, wakimsaidia kusheherekea hatua hii muhimu.
Lulu alionekana aking'ara kwa furaha, akipokea pongezi na zawadi kutoka kwa wageni huku Edwin akieleza jinsi anavyofurahia kuanza maisha mapya na Lulu, huku akiwashukuru wote walioweza kuhudhuria.
Sendoff hii imeleta pamoja familia na marafiki, ikiashiria upendo na mshikamano. Ni mwanzo mpya wa safari ya pamoja huku kila mmoja akitazamia siku ya harusi kwa matumaini na furaha isiyopingika!
Social Plugin