Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : DIWANI WA KATA YA ITWANGI SONYA JILALA MHELA AFARIKI DUNIA

 

Diwani wa kata ya Itwangi Sonya Jilala enzi za uhai wake

****
Diwani wa kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Sonya Jilala Mhela amefariki dunia.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje amesema Sonya alifariki dunia juzi kwa ajali ya pikipiki.

"Tumepoteza kiongozi mahiri, alipata ajali ya pikipiki akavunjika mguu wakati anaendelea kupata matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza Presha ikapanda akafariki dunia..Mazishi yanafanyika leo Jumatatu Oktoba 7,2024 nyumbani kwao Itwangi", amesema Ngassa Mboje.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com