RAIS SAMIA AWAPA FURAHA WAKULIMA WA KOROSHO KILO 1 YAFIKA TSH 4120


 
Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2024-2025 umefanyika kupitia chama kikuu cha ushirika cha TANECU kinachohudumia wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara. 

Jumla ya tani 3,857 za korosho ghafi ziliuzwa kwa kutumia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX) Bei ya juu iliyofikiwa ni shilingi 4120 kwa kilo na bei ya chini ni shilingi 4,035 kwa kilo kutoka bei ya shilingi 2500 kwa kilo. 

Wakulima wa kutoka Tandahimba na Newala wanaishukuru serikali ya Rais Samia  kwa kusikia kilio chao kwa bei nzuri ambayo haijawahi kutokea  kwani kwa miaka kadhaa nyuma bei haikuwa nzuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post