Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limekutana na Wateja wakubwa wa umeme wakiwemo Wamiliki wa Viwanda na Migodi lengo likiwa ni kuwashukuru pamoja na kusikiliza na kupokea maoni ili kuboresha huduma za umeme kwa wateja.
Kikao hicho kilichokutanisha Wateja wakubwa wa umeme mkoa wa Shinyanga kimefanyika leo Alhamisi Oktoba 3,2024 katika ukumbi wa The Planet Hotel Mjini Kahama ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Katika kikao hicho, TANESCO imetoa tuzo na vyeti vya shukrani kwa wateja wanaolipa Ankara kubwa na kwa wakati huku ikiwashukuru wateja wake wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuchangia mapato katika shirika hilo.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, CP Hamduni ameipongeza TANESCO Mkoa wa Shinyanga
kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuwasambazia wananchi umeme ambapo mpaka sasa jumla ya wateja 98,716 wameshaunganishiwa umeme, kati ya hao wateja wakubwa ni 110.
“Sote tunatambua TANESCO Mkoa wa Shinyanga imeendelea kuimarisha huduma za umeme vijijini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jumla ya vijiji 442 kati ya 506 vimefikiwa na umeme. Ni matarajio ya Serikali kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 vijiji vyote vilivyobaki (64) vitakuwa vimefikiwa na miundombinu ya umeme”,ameongeza CP. Hamduni.
Ameeleza kuwa, pamoja na Mradi wa REA, Serikali imekamilisha mradi wa kusambaza umeme kwenye viwanda na migodi midogo ambapo mpaka sasa maeneo 36 ya wachimbaji wadogo yamenufaika na mradi huo ambapo miongoni mwa maeneo hayo ni Mwakitolyo, Masengwa na Itilima; na Mradi wa kusambaza umeme kwenye vituo vya afya na visima vya maji ambapo Jumla ya vituo vya afya 10 na visima vya maji 12 vimenufaika na mradi huu.
Amebainisha kuwa, kutokana na mahitaji ya umeme kuongezeka, Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa jua unaotekelezwa katika kijiji cha Ngunga, Wilaya ya Kishapu wenye thamani ya shilingi 323,059,197.30 ambapo lengo la ujenzi wa mradi huu ni kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Shinyanga, pamoja na nchi kwa ujumla na kwamba Mradi huo unatarajiwa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150.
“Serikali kupitia Shirika la Umeme TANESCO inakamilisha mradi wa kuongeza hali ya upatikanaji wa umeme kwa kuongeza mashineumba (transfoma) yenye ukubwa wa 120/90MVA kwenye kituo cha kupoza umeme wa grid cha Bulyanhulu. Kwa kuzingatia hatua hizi, niseme wazi kuwa TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limejipanga vizuri kuhakikisha wateja wanapata huduma ya umeme wa uhakika ili kutokutatiza utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uchumi, huduma za kijamii pamoja na matumizi ya kawaida katika jamii hasa wakati huu wa kampeni ya matumizi ya nishati safi katika Taasisi na kaya zetu”,ameongeza CP. Hamduni.
Amewaomba wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kulipa Ankara za kila mwezi na kwa wakati ili kuendelea kuwezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiutendaji ndani ya Shirika.
“Niziombe sana Taasisi na Mamlaka za Maji hapa Mkoani ambao ni wadaiwa wakubwa wajitahidi kupitia vyanzo vyao kulipa madeni wanayodaiwa ili kuiwezesha TANESCO kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa ubora uliokusudiwa”,amesema.
“Tunayo kila sababu ya kuipongeza Serikali yetu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na kuweza kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kuifanya huduma ya umeme hapa Nchini izidi kuimarika. Sote tunatambua tulikotoka na tunakoelekea, kukatika kwa umeme au mgao wa umeme unaelekea kuwa historia”,ameongeza CP. Hamduni.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe amewashauri Wateja wa Umeme kurekebisha mifumo yao ya umeme kwenye maeneo yao ili waweze kulipa bili halisi kulingana na matumizi ya umeme.
“ Tunataka muimarishe mifumo yenu ya umeme ili kupunguza malalamiko ya ongezeko la bili za umeme, rekebisheni mifumo yenu ili mulipe pesa kulingana na huduma mnazopata, tunataka tuwatoze fedha kulingana na matumizi halisia”,ameeleza Mhandisi Mwakatobe.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe (kulia).
“Sasa hivi tuna umeme wa kutosha, ukiona umeme umekatika ujue tu kuna changamoto zingine. Wawekezaji endeleeni kuwekeza, wekezeni umeme upo wa kutosha, na kama kuna mwekezaji anahitaji miundombinu tupo tayari kumwekea miundombinu kama uwekezaji wake ni mkubwa au kama mnataka kuboreshewa hii iliyopo njooni tuzungumze tuwawekee miundombinu ya umeme”,amesema Mhandisi Mwakatobe.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Mwakatobe amesema TANESCO inaendelea kuweka nguzo za zege ili kukabiliana na changamoto za mvua ili miundombinu iwe imara lakini pia kuongeza Laini kwa wateja mfano sasa Jambo wanamjengea Laini yake ili kupunguza athari za kukatika kwa umeme na kwamba wanaendelea kuboresha mifumo yao ili umeme usitikisike na kusababisha hasara kwa wateja.
Katika hatua nyingine amesema katika mwaka huu wa fedha TANESCO Mkoa wa Shinyanga imetengewa shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya miradi ya umeme ili kuhakikisha kuna upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mwandamizi TANESCO Makao Makuu, Salama Kasamalu amewasisitiza wawekezaji kuendelea kuwekeza kwani Umeme katika Gridi ya Taifa upo wa kutosha na Miradi mbalimbali ya Kimkakati inaendelea kutekelezwa ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya Nishati safi.
Naye Meneja wa Huduma kwa wateja TANESCO Makao Makuu, Said Mrema amesema TANESCO inaendelea kuboresha huduma ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora ikiwemo Kituo cha huduma kwa wateja kimeboreshwa, mfumo wa Nikonekti na wanaendelea na maboresho ya mifumo ili kuhakikisha huduma kwa wateja zinawafikia wateja kwa wakati.
Aidha amesema TANESCO itajitahidi kuendelea kukutana na wateja wake wakubwa ili kujua matatizo yao na kuwatafutia ufumbuzi.
Nao Wadau hao wakubwa wa umeme wameomba kuwe na punguzo la bei ya umeme, kumaliza tatizo la umeme kukatika ghafla kwamba endapo wakitaka kukata umeme watoe taarifa kwani viwanda, migodi inapata hasara pindi umeme unapokatika.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwenye Kikao cha TANESCO Mkoa wa Shinyanga na Wadau Wakubwa wa Umeme mkoani humo leo Alhamisi Oktoba 3,2024 Mjini Kahama - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza kwenye Kikao cha TANESCO Mkoa wa Shinyanga na Wadau Wakubwa wa Umeme mkoani humo.

Meneja wa Huduma kwa wateja TANESCO Makao Makuu, Said Mrema akizungumza kwenye Kikao cha TANESCO Mkoa wa Shinyanga na Wadau Wakubwa wa Umeme mkoa wa Shinyanga

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye Kikao cha TANESCO Mkoa wa Shinyanga na Wadau Wakubwa wa Umeme mkoa wa Shinyanga

Afisa Uhusiano Mwandamizi TANESCO Makao Makuu, Salama Kasamalu akizungumza kwenye Kikao cha TANESCO Mkoa wa Shinyanga na Wadau Wakubwa wa Umeme mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni (kulia) akikabidhi tuzo kwa wateja wanaolipa Ankara kubwa ya umeme na kwa wakati

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akipiga picha na wateja wanaolipa Ankara kubwa ya umeme na kwa wakati waliopewa tuzo
Zawadi kwa wadau wa umeme
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni (kulia) akikabidhi vyeti kwa wateja wanaolipa Ankara kubwa ya umeme na kwa wakati

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akipiga picha na wateja wanaolipa Ankara kubwa ya umeme na kwa wakati waliopewa vyeti

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akipiga picha na wateja wa TANESCO

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akipiga picha na wafanyakazi wa TANESCO
Wateja wakubwa wa TANESCO wakiwa ukumbini

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin