WASIOJULIKANA WAWASHA MOTO SHAMBANI, WAUNGUZA NGUZO ZA UMEME, TANESCO SHINYANGA YATANGAZA KATIZO LA UMEME

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoani Shinyanga linaomba radhi wateja wake kwa kukosekana kwa huduma ya Umeme katika baadhi ya Maeneo ndani ya Mkoa Wake.

Muda: ni Kuanzia saa 8:15 Usiku Mpaka sasa.

Sababu:  Moto Uliozuka Eneo la Seseko Mashambani na kupelekea nguzo mbili za usafirishaji umeme kuungua na kuanguka.

Maeneo yanayoendelea kuathirika ni

Uzogole, Ning’wa, Chibe, Butengwa, Mwalugoye, Old Shinyanga, Mwalukwa, Pandagichiza, Mwamakaranga, Nindo, Bukambe, Nyamalogo, Shatimba, Mwang’osha, Lyabusalu, Nzumve pamoja na Mwapangabule, Seseko.

Jitihada za Kubadili Nguzo hizo zinaendelea pamoja na kuwatafuta waliosababisha uharibifu huu katika miundombinu ya Umeme.

RAI KWA WANANCHI:  TUNAOMBA WANANCHI WAZINGATIE SWALA LA USALAMA WA MIUNDOMBINU YA UMEME WANAPOENDELEA NA SHUGHULI MBALIMBALI IKIJUMUISHA USAFISHAJI WA MASHAMBA KWANI ULINZI WA MIUNDO MBINU YA UMEME NI JUKUMU LETU SOTE.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza kutokana na katizo hili.

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa TANESCO kwa simu namba 0748 550 000 au 0733 105 423.

*IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA TANESCO - SHINYANGA.*

05.10.2024

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post