Kishindo cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye elimu kimeendelea kuwagusa wananchi baada ya kuweka kiasi cha Shilingi 585,280,028/= kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kisasa ya Sekondari wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Shule hiyo ya Kata ya Mwanuzi ina madarasa nane, jengo la Utawala, Maabara tatu, vyoo 10, chumba cha Kompyuta, Maktaba na sehemu maalum ya kuchomea takataka.
Uzinduzi wa mradi huo ulifanywa jana Oktoba 27,2024 na
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa niaba ya Rais Dkt Samia.
#KAZI INAONGEA
Social Plugin