RAIS SAMIA AMLILIA MUSUGURI

 


Mkuu wa Majeshi wa zamani Tanzania, Jenerali David Musuguri amefariki Dunia

Mkuu wa Majeshi wa zamani Jenerali David Musuguri, amefariki Dunia, Oktoba 29, 2024, jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Jenerali Musuguri, aliyezaliwa Januari 4, 1920 aliitumikia nchi katika Jeshi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988.

Jenerali Musuguri aliongoza majeshi ya Tanzania katika vita dhidi ya Idi Amin Dada wa Uganda Mwaka 1978, baada ya uvamizi wa eneo la Kyaka, Mkoani Kagera.

Jenerali Musuguri, pia alishiriki katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, na Battle of Simba Hills


"Kwaheri, Jenerali.

Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Makamanda, wapiganaji wastaafu, wapiganaji walio katika utumishi, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wetu, mpendwa wetu, mwalimu, mshauri na kiongozi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri. 

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake ya miaka 104, ambapo miaka 46 kati ya hiyo ameitumikia nchi yetu kwa weledi, umahiri, kujituma, ushujaa, nidhamu na kwa mafanikio ya hali ya juu, akiishi kiapo chake cha kuwa tayari kuutoa uhai wake ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Ametuachia mfano bora wa utumishi wa umma utakaoendelea kuwa mwanga ndani na nje ya Majeshi yetu. 

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. 

Amina" _ RAIS SAMIA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post