MARIAM ULEGA AONGEZA NGUVU USAJILI WA WANACHAMA KIELEKTRONIKI CCM – UWT SHINYANGA MJINI

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (wa pili kulia) akikabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega amechangia Simu Janja tatu ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Ndugu  Mariam Abdallah Ulega ametoa msaada huo leo Jumatatu Oktoba 7,2024 kwenye Kikao cha Viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakati akiwa ziara yake ya Kuhamasisha zoezi la kusajili wanachama wa CCM Kielektroniki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha CCM.

“Sisi wote wanaCCM ni ndugu, tunaimarisha chama chetu na tunaendelea kukijenga zaidi. Kwa kasi yenu ya Usajili hapa ninavyoiona na nguvu kubwa mnayotumia kuhakikisha tunapata wanachama wengi zaidi katika chama chetu cha Mapinduzi, Na mimi nimewiwa kuongeza nguvu kwa UWT, nakabidhi simu hizi tatu ili tuendelee na zoezi la usajili kwa wale ambao bado hawajajisajili Kielektroniki”,amesema Mariam.

 “Lakini nataka niwaambie viongozi wenzangu hima hima twende tukahimizane tujiandikishe na tuhakikishe tunaboresha taarifa zetu katika Daftari la Wapiga kura,  wale ambao hawajiandikisha kwenye daftari wakati ni sasa daftari lipo, tuzidi kuhakikisha tunakuwa na viongozi bora ambao watakuja kuchukua fomu katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo tunakuwa na wanachama ambao wapo hai na wapo kindakindaki kukipigania chama chetu”,ameongeza Mariam.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe ,Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Hassan Chacha na  Katibu wa UWT Shinyanga Mjini Getrude Mboyi wamemshukuru Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Mariam Abdallah Ulega kwa kuwaongezea nguvu kwa kuwapatia vitendea kazi huku wakieleza kuwa zoezi la kusajili Kielektroniki wanachama CCM linaendelea vizuri.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (wa pili kulia) akikabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. Kushoto Katibu wa CCM Shinyanga Mjini, Hamisa Hassan Chacha akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Mjini, Anord Makombe, kulia ni Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Getrude Mboyi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (kulia) akikabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akizungumza wakati akikabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Katibu wa CCM Shinyanga Mjini, Hamisa Hassan Chacha akitoa neno la shukrani kwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega baada ya kukabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akitoa neno la shukrani kwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega baada ya kukabidhi Simu tatu kwa viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ili kuongeza nguvu ya Kusajili Kielektroniki Wanachama wa CCM kupitia UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini. 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Mjini, Anord Makombe baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye kikao
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye kikao
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akiagana na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu akizungumza jambo wakati wa ziara ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega Mkoa wa Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akiondoka katika ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post