KISHINDO CHA BALOZI NCHIMBI SHINYANGA...ATOA MAELEKEZO KWA MAWAZIRI MAOMBI YA MBUNGE KATAMBI




Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa maelekezo kwa Mawaziri wawili, juu ya maombi ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza leo Oktoba 11,2024 kwenye Mkutano wa Dk.Nchimbi, ametoa maombi kwake, kwamba Kata ya Ibadakuli inahitajika kujengwa kituo cha afya, kuongezwa fedha za ukarabati hospitali ya manispaa ya Shinyanga, ukarabati wa miundombinu ya barabara katika mitaa yote ambazo ziliharibiwa na mvua, pamoja na utatuzi wa mgogoro baina ya Jeshi na wananchi.

Awali Katambi akizungumza kabla ya kutoa maombi hayo, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, imetoa fedha nyingi jimboni humo, na miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa ukiwamo ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli,miundombinu ya barabara na madaraja.
Amesema Rais Samia pia ameboresha huduma za afya katika manispaa ya Shinyanga ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya, hospitali, pamoja na zahanati mpya 7 ikiwamo na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.

“Tunakuomba umefikishie Rais wetu salamu nyingi sana za wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini, kwa kututekelezea miradi mingi ya maendeleo,”amesema Katambi.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza kwenye mkutano huo, amempongeza Mbunge Katambi kwa kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo, chini ya Daktari Rais Samia Suluhu Hassan, na kwamba maendeleo yaliyopo shinyanga yanaonekana kwa macho wala haihitaji tochi wala darubini, na atakaye pinga apelekewe hospitali ya milembe akapimwe akili.

“Hapa Shinyanga mmepata maendeleo makubwa, na zawadi yenu kwa Rais Samia ni kumpatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani 2025,”amesema Dk.Nchimbi.
Aidha, akijibu maombi ya Mbunge Katambi,ametoa maelekezo kwa Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kwamba kuhakikisha ana kijenga kituo cha afya Ibadakuli, pamoja na kutoa fedha kukamilisha ukarabati wa hospitali ya manispaa ya Shinyanga.

Ameelekeze tena Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa pamoja na Waziri wa Ulinzi Dk Stergomena Tax washirikiane ili kutatua Mgogoro baina ya Jeshi na wananchi, huku akiagiza TARURA kufanya ukarabati wa ujenzi wa barabara katika mitaa ya manispaa ya Shinyanga.
Katika hatua nyingine amewahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ambalo limeanza leo Oktoba 11 na kutamatika tarehe 20, ili wapate fursa ya kupiga kura Novemba 27, na kuchagua viongozi wazuri kutoka CCM, na kwamba Rais Samia tayari yeye ameshajiandikisha.

Pia, amewataka wananchi waendelee kudumisha Amani ya nchi, na wasikubali kuivuruga kwa maslahi ya watu wachache.
Katibu wa Itikadi, Siasa,Uenezi na Mafunzo Amosi Makala, amesema yeye amewahi kuishi Shinyanga, na kwamba Shinyanga ya zamani siyo ya sasa sababu imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi, imetamatika leo mkoani Shinyanga, ambapo ili lenga kukagua uhai wa Chama, kuangalia utekelezaji wa ilani, pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu wakiteta jambo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Rabia Abdalla (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Katibu wa Itikadi, Siasa,Uenezi na Mafunzo Amosi Makala akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Rabia Abdala akizungumza kwenye mkutano huo.
Mchungaji Peter Msingwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye mkutanoi huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akifurahia na wananchi kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post