CPA RITHAMARY LWABULINDA KUFUATILIA HUDUMA YA MAJI MAPINGA
Thursday, October 31, 2024
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja ,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) CPA(T) Rithamary Lwabulinda amekagua hali ya upatikanani wa huduma katika Mkoa wa kihuduma DAWASA Mapinga na kuongea na Wateja wa Mamlaka ili kubaini changamoto zao za kihuduma.
Ametembelea eneo la Kilemela ambapo kulikuwa na changamoto ya huduma iliyosababisha Wananchi kukosa huduma ya maji na kushuhudia maboresho ya Miundombinu ikiendelea ya ufungaji wa pampu itakayosaidia kuongeza msukumo wa maji kwa wateja takribani 73 waliokuwa wanapata maji kwa kiwango kidogo.
DAWASA Mapinga inahuduma wananchi wa Kata za Mapinga, Kerege na Pangani zenye jumla ya Vitongoji 19 na wakazi 87,418
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin