eGA YAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA KWA KUSANIFU NA KUSIMAMIA MIFUMO YA TEHAMA NCHINI

 


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama (aliyekaa meza kuu) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyesimama) alipokuwa akitoa shukrani kwa kamati hiyo baada ya kumaliza kikao kazi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo na taasisi zake kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Taasisi ya UONGOZI ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba akijibu hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akijibu hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Lutechura Kiliba akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa kwa taasisi anayoisimamia wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo na taasisi zake kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akijibu hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akifafanua hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi akijibu hoja ya taasisi anayoisimamia kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Sehemu ya Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.


Na. Veronica Mwafisi-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia taasisi iliyopo chini yake ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kusanifu na kusimamia mifumo mingi ya TEHAMA nchini ili kuboresha utoaji huduma kwa taasisi za umma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Taasisi ya UONGOZI iliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa tassisi hizo.

Mhe Mhagama amesema ni wazi kuwa kwa sasa taasisi zote za serikali zinatumia mifumo ya TEHAMA hivyo, eGA ina wajibu wa kuzisaidia taasisi hizo ili kutimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na serikali ya kidijitali itakayokidhi mahitaji na viwango vikubwa katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Tunafahamu kuwa kila taasisi ya serikali inatumia mifumo ya TEHAMA, niwasihi endeleeni kushirikiana ili kuleta tija na manufaa katika utendaji kazi kwa lengo la kutimiza malengo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na serikali ya kidijitali kwa maendeleo ya nchi yetu. Dkt. Mhagama amesisitiza

Akizungumzia maeneo ambayo jiografia yake haipo vizuri, Mhe. Dkt. Mhagama amesema maeneo hayo yanapaswa kuwa na miundombinu ya TEHAMA itakayowezesha upatikanaji wa huduma za kimtandao uliosanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ili kuwasaidia watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao bila kuwa na changamoto ya kimtandao.
Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Mhagama ameipongeza Taasisi ya UONGOZI kwa kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa viongozi jambo ambalo linawasaidia watumishi katika taasisi mbalimbali kuwajibika kwa ufasaha kupitia mafunzo ambayo wamekuwa wakipatiwa kutoka katika taasisi hiyo.

Ameisisitiza taasisi hiyo kuendelea kuwajengea uwezo viongozi waliopo ili kuwa na viongozi bora na wazalendo kwa nchi yetu.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kutoa ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo ofisi yake imekuwa ikiifanyia kazi na kwa asilimia kubwa imeisaidia ofisi hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Mhe. Mwenyekiti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora inajivunia kusimamiwa na Kamati yako kwani mmekuwa mkitupatia ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo yameleta tija kwetu na kutufanya tutekeleze majukumu yetu kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa sana. Mhe. Simbachawene amesema.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imemaliza kikao kazi chake cha siku mbili kwa kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na baadhi ya taasisi zake ikiwemo TASAF, eGA na Taasisi ya UONGOZI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post