EWURA YACHANGIA MADAWATI KWA WANAFUNZI 150 SHULE YA MSINGI KILOLENI

 

Mkuu wa Shule ya Msingi Kiloleni, Rajabu Kiama (kulia) akiishukuru EWURA kwa kuwezesha ununuzi wa madawati yaliyokabidhiwa shuleni hapo na Ofisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Bi Getrude Mbiling’i (wa pili kushoto) leo 11/10/24. Anayeshudia kushoto ni mtumishi wa EWURA wa Kanda hiyo, Elly Mmbaga.

........

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, leo, 11/10/24, imekabidhi madawati 50 yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi 150 wa shule ya msingi Kiloleni yenye usajili P1903011 iliyopo manispaa ya Tabora.

Mkuu wa Shule hiyo, Rajabu Kiama ameishukuru EWURA kwa kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule hiyo.

“Uongozi wa shule unatoa shukrani kwa EWURA kuunga mkono juhudi za kutatua changamoto hii ya upungufu wa madawati kwa wanafunzi, ambayo yatawapa fursa wanafunzi 150 kukalia madawati”, alisema

Ofisa Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Getrude Mbiling’i, akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Mamlaka, amewaasa wanafunzi wa shule hiyo kutunza samani walizopatiwa.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme, gesi ya kupikia na utaratibu wa EWURA wa kushughulikia malalamiko yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa katika sekta za nishati na maji.

Kiloleni ni miongoni mwa shule kongwe iliyopo Kata ya Mapambano, Halmashauri ya Tabora na ilianzishwa mwaka 1970. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1050; wavulana 520 na wasichana 530 na jumla ya walimu 13.

Mkuu wa Shule ya Msingi Kiloleni, Rajabu Kiama (kulia) akiishukuru EWURA kwa kuwezesha ununuzi wa madawati yaliyokabidhiwa shuleni hapo na Ofisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Bi Getrude Mbiling’i (wa pili kushoto) leo 11/10/24. Anayeshudia kushoto ni mtumishi wa EWURA wa Kanda hiyo, Elly Mmbaga.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiloleni ya mkoani Tabora, wakiwa na machapisho mbalimbali ya EWURA baada ya kupata elimu kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme, gesi ya kupikia na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko EWURA kuhusu huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka kutoka kwa maofisa wa EWURA wa Kanda ya Magharibi,.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiloleni ya Tabora, wakiwa wameketi katika madawati yaliyokabidhiwa na EWURA Kanda ya Magharibi, shuleni hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post