GCLA YAWATAKA WAUZAJI NA WAAGIZAJI WA RANGI NCHINI KUZINGATIA MAELEKEZO KUDHIBITI SUMU ITOKANAYO NA MADINI YA RISASI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kupitia kituo chake cha kudhibiti matukio ya sumu, kimewataka  wazalishaji na  waingizaji wa rangi nchini kuhakikisha wanazingatia maelekezo waliyopewa ili kudhibiti sumu itokanayo na madini ya risasi kwa lengo la kuzuia athari .

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25,2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali Daniel Ndiyo kwenye mkutano uliowakutanisha wadau katika tasnia ya rangi ambapo umekusudia kuimarisha ushirikiano katika pande zote kwa dhumuni la kuhakikisha usalama kwa jamii.

"Rangi imekuwa ikitumika kupaka kwenye mabati ambapo watu katika kipindi cha mvua  hutumia maji hayo ikiwa uhakika wa usalama wake kwa matumizi haujulikani". Amesema 

Aidha ametoa rai kwa wadau wanaohusika kwenye tasnia ya rangi,kuondokana na dhana potofu ambayo imezoeleka,kutumia  maziwa pekee kwa ajili ya kudhibiti sumu mwilini kwani inaweza kudhibiti baadhi ya sumu chache pekee  na sio zote  Kama ilivyo zoeleka.

Kwa upande wake mdau Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalam ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu Prof. Amos Mwakigonja amewaagiza watu wanaoshughulika na kazi zinazohusiana na madini ya risasi  kuunga juhudi zinazofanyika kwakuachana na shughuli ambazo zinahusiana na usambazaji wa madini hayo katika mazingira,ambapo itasaidia kuepusha madhara kwa watu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post