Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AELEKEZA MAKAMPUNI YA MADINI KUCHANGIA NA KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA VETA GEITA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyaelekeza makampuni ya madini kuchangia na kushirikiana na chuo cha VETA Geita katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi.

Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo hayo alipotembelea wakati akifunga Maonyesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini, jana, tarehe 13 Oktoba, 2024.

Mhe. Rais amesema ushirikiano huo pia uwawezeshe vijana kujifunza na baada ya kuhitimu wafanye kazi kwenye makampuni ya madini yaliyopo ndani ya mkoa wa Geita.

Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Martin Shigella kuratibu suala hilo na kuhakikisha linatekelezwa.

Chuo cha VETA Geita ni chuo cha hadhi ya mkoa ambacho kimeanza mafunzo mwaka 2024 na kina uwezo wa kudahili wanafunzi 720 kwa kozi ndefu na kozi fupi 1500 kwa mwaka na kwa sasa chuo kinatoa mafunzo katika fani za Umeme na Bomba, na chuo kinatarajia kutoa zaidi ya fani 13 katika maeneo mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com