Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA KEKO HADI KIVULE

 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA - Temeke umeendesha zoezi la kugawa na kutoa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi ambapo leo tarehe 29/10/2024 umekabidhi vifaa kwa wateja 12 wa maeneo ya Keko, Buza, kigilagila, Sandali, Tandika, Kerezange na kivule


Aidha kupitia zoezi hilo elimu mbalimbali zimeendelea kutolewa ikiwemo utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji na njia rasmi za malipo ya kiserikali, njia za mawasiliano na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Kwa msaada wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0737-730523 (DAWASA Temeke).



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com