KAMA HAUNA SIFA USICHUKUE FOMU YA KUGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA:RC MWASSA




Na Mariam Kagenda _Kagera


Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewatahadharisha watu wasio na sifa za kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa hususani wahamiaji haramu, kutothubutu kuchukua fomu na wakibainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria. 

Hajatil Mwassa amesema hayo wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwakwe wakati akitoa taarifa kwa Umma juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchi nzima Novemba 27 mwaka huu.

"Sisi mkoa wetu uko mpakani tunajua kabisa kuwa wapo watu ambao wameingia hapa nchini na wengine wamebaki bila kutoka hivyo wanaishi kinyume cha sheria na taratibu za nchi na wangependa kuwa viongozi na wengine wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo rushwa ili wachaguliwe kuwa viongozi wakijaribu kugombea tutawachukuli hatua za kisheria"
Aidha amewatahadharisha wananchi wa Kagera kutochagua watu ambao si watanzania kwani uchaguzi huu ni kwa ajili ya watanzania pekee hivyo mwenye haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni mtanzania tusiweke mamluki kwenye nchi yetu tusilete hatari na kusababisha hatari ndani ya nchi yetu.

Amesema mkoa wa Kagera unakadiliwa kuwa na watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wapatao milioni 1.5 wanawake wakiwa laki 7.5 na wanaume laki 8.2 ambapo vipo vituo vya uandikishaji wapiga kura 3,833 hivyo amewashauri wananchi kujitokeza kujiandikisha ili wapate fursa ya kutumia haki yao ya msingi na kikatiba ya kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi.

Alisema uandikishaji utaanza Oktoba 11 hadi 20
mwaka huu huku zoezi la kuchukua na kurejesha form likianza Novemba mosi hadi saba mwaka huu.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post