KIKUNDI RAFIKI CHA MAZINGIRA KUCHAGIZA USAFI WA MAZINGIRA BUGURUNI

 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Buguruni Kisiwani wameunda kikundi rafiki cha mazingira katika jitihada za kuchagiza usafi wa mazingira katika eneo hilo.


Hatua hii inafanyika baada ya maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Edward Mpogolo kwa DAWASA alipotembelea eneo hilo kuhakikisha inashirikiana na jamii ya Buguruni Kisiwani katika uendeshaji wa mradi wa mfumo rahisi wa uondoshaji majitaka majumbani.

Akizungumza katika kikao na wananchi Diwani wa Kata ya Buguruni Mh. Busolo Pazi ameeleza kuwa katika uendeshaji wa miradi kama huu, DAWASA, wananchi na viongozi kila mmoja anajukumu la kufanya ili kuona mradi unaleta tija kwa wananchi na unasaidia kuboresha mazingira katika mtaa wao.

"Niwaombe wananchi tuwe walinzi wa kwanza wa miundombinu ya majitaka, tusiwe sababu ya miundombinu hii kuziba na kutokufanya kazi, sehemu zenye changamoto katika mradi huu DAWASA wanaenda kuzifanyia kazi" ameeleza Mh.Pazi

Kwa upande wake Meneja wa huduma za majitaka DAWASA, Mhandisi Jolyce Mwanjee ameeleza kuwa kuundwa kwa kikundi hiki ni mwanzo mzuri wa ushirikiano baina ya wananchi wanufaika na DAWASA unaolenga kutatua changamoto zote za uchafuzi wa Mazingira zilizojitokeza katika eneo hilo.

Nae Afisa maendeleo ya Jamii ndugu Elizabeth Eusebius ameelza kuwa Mamlaka itashirikiana bega kwa bega na kikundi hiki Ili kuhakikisha wanatatua changamoto zote za uchafuzi wa mazingira Buguruni kisiwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post