KITUO CHA AFYA SEGESE KIANZE KAZI IFIKAPO MWEZI OKTOBA - WAZIRI NDEJEMBI

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Deogratius Ndejembi akitembelea  kituo cha afya Segese Halmashauri ya Msalala 


NA NEEMA ISRAEL - MSALALA


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Deogratius Ndejembi amemtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kuhakikisha kituo cha afya Segese kinaanza kufanya kazi mara moja kwani jengo la OPD tayari limekamilika na vitendea kazi vya kuanzia vipo.


Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo leo Oktoba 6, 2024 alipotembelea kituo cha Segese na kubaini baadhi ya mapungufu ambapo amesema watumishi wanatumia mianya kutokukamilika kwa majengo kupiga fedha za mapato ya ndani.


Aidha Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha amewataka Wahandisi wakabidhi majengo yanayolingana na thamani ya fedha zinazotolewa.


Akisoma taarifa za ujenzi wa kituo hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha amesema Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2022 kupitia mapato ya ndani shilingi 470,000,000/= baada ya wananchi wa Kata Segese kukosa huduma za afya ambapo walianza na ujenzi wa majengo manne, jengo la wagonjwa wa nje OPD, Maabara, Upasuaji na jengo la mama na mtoto.


Ujenzi wa jengo la OPD limegharimu kiasi cha 208,839, 549.9 ambapo umekamilika kwa asilimia 96 na asilimia zilizobaki ni kuingiza umeme, maji na thamani.


Kituo hicho kikikamilika kinatarajiwa kuhudumia wakazi 36,247 wa Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala.



Jengo la mama na mtoto lililokamilika kwa asilimia 70 na kugharimu shilingi 77,501,992.32
Majengo ya maabara na OPD ambayo yamekamilika kwa asilimia 96 ambapo jengo la maabara limegharimu 96,957,632.58 na jengo la wagonjwa wa nje OPD limegharimu 208,839,549.9
Waziri Ndejembi akizungumzia suala la kituo cha afya kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi waanze kupata huduma za afya ifikapo mwezi wa 11
Waziri Ndejembi akizungumzia suala la kituo cha afya kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi waanze kupata huduma za afya ifikapo mwezi wa 11

Mkuu wa mkoa Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha afya Segese ambapo amewataka wahandisi kukabidhi majengo kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa
Mkuu wa mkoa Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha afya Segese ambapo amewataka wahandisi kukabidhi majengo kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post