Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani baada ya kuipokea meli iliyotoka nchini China moja kwa moja kuleta shehena ya magari kupitia kampuni ya Meli ya SeaFront Shipping Services Limited (SSS).
Afisa Uhusiano wa TPA Enock Bwigane akizungumza wakati wa mapokezi ya meli hiyo
Na Oscar Assenga,TANGA
MATUNDA ya Uwekezaji wa Bandari ya Tanga wa Sh.Bilioni 429
uliofanywa na Serikali umeanza kulipa kutokana na maboresho makubwa na hivyo
kuwezesha ongezeko kubwa la idadi ya meli zinazopitisha shehena kutoka meli 197
kwa mwaka 2022/2023 hadi kufikia meli 307 kwa mwaka 2023/2024
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud
wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuipokea meli ya XINHAITONG 50 iliyotoka
nchini China moja kwa moja kuleta shehena ya magari kupitia kampuni ya Meli ya SeaFront
Shipping Services Limited (SSS).
Alisema ujio wa meli hizo kushusha magari katika Bandari hiyo
inadhihirisha kwamba ufanisi mkubwa katika shughuli za kupakia na kupakua
zimeimarika kutokana na maboresho hayo makubwa.
“Lakini niseme kwamba maboresho haya pia yameleta ongezeko kubwa
la ajira na hadi sasa idadi ya makampuni ya wakala wa usafirishaji katika
bandari yameongezeka kutoka 32 hadi 132”Alisema
Akizungumzia kuhusu ongezeko la mapato katika Bandari hiyo
alisema kwamba yameongezeka ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Bandari
ilikusanya mapato ya Sh.Bilioni 16 lakini kwa mwaka 2023/2024 mapato hayo
yameongezeka hadi Sh.Bilioni 18.6 ikiwa ni ongezeko la asilimia 74.1.
“Ongezeko hilo la mapato
linatokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari ya Tanga,na ni muhimu kwa
maendeleo ya uchumi wa nchi kwa ujumla “Alisema
Alisema kwamba maboresho haya yanaonyesha jinsi uwekezaji katika
miundombinu unavyoweza kuleta matokeo chanya kwa jamii na uchumi wa Taifa.
Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha
sekta ya usafirishaji ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kitovu cha biashara
katika eneo la Afrika Mashariki.
Awali akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Afisa Uhusiano wa
TPA nchini Enock Bwigane amesema wan mshukuru mdau wa kampuni ya Sea Front ambaye
amefanikisha kuwasili kwa meli hiyo iliyobeba shehena mchanganyiko yakiwemo
magari zaidi ya 350.
Bwigane alisema kwamba asilimia
kubwa ya shehena hiyo inaelekea nje ya nchi na kuwepo kwa meli hiyo ambayo
inahudumiwa kwa saa 48 tangu ifike leo alfariji inafikisha meli idadi ya meli
12 ambazo zimehudumiwa na mteja wao Kampuni ya Sea Front Shipping.
Alisema kwamba mteja wao huyo
alikuwa akifanya huduma za kibandari katika Bandari ya Dar lakini kutokana ana
uwekezaji uliofanywa na Serikali wa Bilioni 429 .1 kwa awamu zote mbili
kuboresha bandari ya Tanga umepelekea meli kubwa nyingi kwa shehena tofaui
kuhudumiwa katika Bandari ya Tanga.
“Huyu ni mteja mojawapo alileta meli
kutoka nchini China na ambapo meli hii imefikisha idadi ya meli 12 ambazo zimeshuhudumiwa
na tunapoongelea ufanisi wa mapato katika Bandari ya Tanga tunajivunia”Alisema
Alisema robo ya kwanza ya Julai Mosi hadi Septemba 30 mwaka huu Bandari hiyo
ilikusanya Bilioni 18.6 na Bilioni 8 katika mapato hayo zimetokana na mteja
huyo ambaye amekwisha kuwezesha ujio wa meli 12 katika Bandari hiyo.
“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu
kwa maamuzi yake ya kufanya maboresho katika Bandari zote nchini ikiwemo
Bandari ya Tanga ambapouwekezaji mkubwa uliofanyika umesaidia kuongeza ufanisi katika
Bandari na mapato yameongezeka na huduma ya shehena zimeongezeka kila mwaka
ukiangalia kwa miaka miwili iliyopita”Alisema
Alisema shehena hiyo imeongezeka
kutoka kuhudumia shehena tani 800,000 na sasa wana Milioni 1.5 na mwaka huu
wanatarajia kuhudumia shehena tani Milioni 1.4 katika robo ya kwanza na wameshahudumia
shehena tani laki 3.3 .
Aidha alisema kwa hiyo wanapiga
hatua kubwa kwenye kuhudumia shehena nyingi katika Bandari ya Tanga na
kuhudumia shehena kwa ushoroba wa Kanda ya Kaskazini na wanafarajikia kwa mara
ya kwanza kwa nchi ya DRC na Zambia mzigo mkubwa unaopita hapo ni Copper ambapo
zaidi ya tani 30,000 zimehudumiwa hapo.
Alisema katika meli hiyo iliyokuja
kuna mizigo mchanganyiko unakwenda Rwanda katika mchanganyiko wao na wao kama
Bandari wanafarijika kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali katika Bandari.
“Tunasema kwamba baada ya uwekezaji
katika Bandari ya Tanga umelipa ni jambo ambalo tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu
na tumefarijika nasi tunamuhaidi kwamba hatutamuangusha tutafanya kazi kwa
bidii na kuongeza mapato ili kuimarisha uchumi wa nchi”Alisema Bwigane
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin