Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma wa Ukonga imeendesha zoezi la kuwaunganishia huduma ya maji safi wateja wapya 31 kutoka katika maeneo mbalimbali ya kihuduma Ukonga.
Zoezi hilo limetekelezwa kwa wananchi hao walioomba huduma ya maji kutoka katika maeneo ya Kata za Pugu Kichangani, Majohe na Gongolamboto ambapo wamepokea vifaa hivyo vya maunganisho ya huduma na zoezi la kuwanganishia linaendelea katika mitaa yao.
Mamlaka inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja wote walioleta maombi ya kupatiwa huduma ya majisafi katika maeneo yote yanayohudumiwa na DAWASA katika Dar es Salaam na Pwani.
Social Plugin