Na Mwandishi wetu,Geita
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameeleza kuwa Sekta ya Madini imestawi kwa kiasi kikubwa chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Chatanda ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya Madini ikiwemo ushirikishwaji na uwezeshwaji wa Wanawake ikiwa ni pamoja kupatiwa leseni na mitaji inayowawezesha kujiinua kiuchumi.
Hayo ameabinisha leo Oktoba 12 alipotembelea Mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bomba mbili Mkoani Geita.
"Tumejionea namna gani maelekezo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa, tumeona vikundi mbalimbali vya Vijana na Wanawake ambao wamewezesha kupatiwa mitaji na leseni kuweza kufanya shughuli zao" amesema Mwenyekiti Chatanda na kuongeza
Hakika hatuna budi kumshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae anawapenda wananchi wake,anataka kila mwananchi awezeshwe kiuchumi, "amesema.
Social Plugin