Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NSSF SHINYANGA YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, MDABI AWAKARIBISHA WACHIMBAJI, BODABODA NA MAMALISHE KUCHANGAMKIA FURSA

Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akikata keki pamoja na Wadau wa NSSF wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 Blog

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi amefungua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata na kula keki na wanachama na wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 7,2024 wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Meneja wa NSSF mkoa wa Shinyanga  Mdabi amesema kuwa wiki ya huduma kwa wateja ilianzishwa rasmi kimataifa mwaka 1987 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja na juhudi za wafanyakazi wanao toa huduma bora kwa wateja.

“Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika kila mwaka kimataifa, NSSF mkoa Wa Shinyanga tunaitumia wiki hii kutafakari juu ya huduma tunazotoa, kusikiliza wateja na wadau mbalimbali,Kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja mwakahuu ni 'Huduma Bora Popote Ulipo',amesema Mdabi.

Mdabi amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mtoa huduma namba moja kwa juhudi kubwa anazo fanya na anazo endelea kuzifanya katika kuhakikisha anaboresha huduma kwa jamii huku akiwaomba wanachama wa NSSF na waTanzania kwa ujumla kuendelea kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na Dkt. Samia.

Aidha Mdabi amewashukuru wanachama wa mfuko wa NSSF mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuwaomba wajasiriamali ,Bodaboda na wachimbaji kujiunga na NSSF Ili waweze kujiwekea Mafao kidogokidogo yatakayo wasaidia uzeeni.

"Pia tuna mshukuru Mkurugenzi mkuu na bodi ya wadhamini kwa namna ambavyo wameweza kuboresha utendaji kazi kwa kutumia Teknoloji hali ambayo kwa sasa imeasaidia kuhudumia wateja kwa ufanisi",amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Shinyanga akiwemo Mary Kabasa na Joseph Kaiula wamesema wataendelea kuwa mabalozi wakutoa elimu kwa watu wengine ambao bado awajajiunga na mfuko huo wakiwemo wajasiriamali na wananchi ili waweze kujiwekea fedha kidogokidogo kwa ajili ya maisha yao ya baadae.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akikata keki wakati wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.
Zoezi la kupongezana likiendelea baada ya ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.Baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi hilo la ufunguzi wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga.
Baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi hilo la ufunguzi wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga.
Baadhi ya wadau wakiwa wameketi pamoja na wafanyakazi wa NSSF kwenye zoezi la ufunguzi wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga.
Baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi hilo la ufunguzi wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga wakishuhudia zoezi la ukataji wakeki katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi hilo la ufunguzi wiki ya huduma kwa wateja NSSF Shinyanga wakishuhudia zoezi la ukataji wa keki katika uzinduzi huo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akilishwa keki na wateja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akimlisha keki mmoja wawafanyakazi wa NSSF wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akiwalisha keki wateja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akiwalisha keki wateja wakati wa uzinduzi wawiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akimpongeza mmoja wa wateja baada ya kufungua Shampeni wakati wa uzinduzi wawiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akiwalisha keki wateja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akiwalisha keki wateja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Zoezi la kupiga picha za pamoja linaendelea baada ya ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com