Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFUKO WA TAIFA WA MAJI YAWEZESHA KUKAMILIKA MIRADI YA MAJI 354 NCHINI


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maji wa Taifa, Wakili Haji Mandule akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika leo, Oktoba 31, 2024, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji Mhandisi Abdallah Mkufunzi akiongea wakati akifafanua baadhi ya Mambo katika kikao kazi hicho.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania, Deodatus Balile, akizungumza kwa niaba ya Wahariri wa vyombo vya habari walioudhuria katika mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri akiongoza majadiliano mara baada ya kutolewa wasilisho kwa Wahariri katika mkutano huo.

PICHA NA; HUGHES DUGILO DAR ES SALAAM.

Afisa Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), Wakili Haji Nandule, amesema, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2024, miradi ya maji 354 kati ya miradi 998 iliyopokea fedha kutoka mfuko huo imekamilika na kunufaisha wananchi wapatao milioni 5.3.

Wakili Nandule amebainisha hayo leo Oktoba 31,2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya wahariri na waandishi wa vyombo vya habari nchini, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Amesema kuwa Mfko huo umefanya kazi kubwa kwa kuhakikisha fedha znazokwenda kwenye taasisi hiyo wanaendelea kuzitoa na kuzielekeza kwenye maeneo husika ili wananchi waweze kupata huduma bora za maji.

"Hii ni taasisi ya fedha yenye lengo la kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya usambazaji maji safi kwenye maeneo yenye uhaba na utunzaji wa vyanzo vya maji nchini.

"Kwa hiyo, kubwa ni kukamilika kwa miradi 354 katika kipindi hicho na hadi kufikia Julai 2024, jumla ya shilingi bilioni 5.3 zimetolewa kama mikopo kwa mamlaka za maji," amesisitiza Wakili Nandule.

Wakili Nandule ameongeza kuwa miradi hiyo inajumuisha uhifadhi wa vyanzo vya maji zaidi ya 92 ikiwemo chemichemi, vidakio vya maji, maziwa,

Aidha amesema, wapokeaji wa fedha za miradi ya mfuko ni Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mamlaka za maji na bodi za maji za mabonde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mfuko wa Taifa wa Maji, Abadallah Mkufunzi amesema katika kipindi cha Miezi sita tangia wameanza kutoa mikopo wamekutana na changamoto mbalimbali ambazo wanazifanyia kazi ili kuzidi kuboresha kanuni walizo nazo

Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania, Deodatus Balile ameushauri mfuko huo kujitangaza mara kwa mara kwa kuzungumza na waandishi wa habari ili jamii iweze kuwatambua.

"Niwaombe mjitangaze kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kufahamu shughuli zenu na miradi mnayotekeleza" amesema Balile

Huduma zinazotolewa na Mfuko zinatokana na majukumu yaliyoainishwa kwenye Sheria katika Kifungu cha 56 ((a) – (g)) kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kusaidia uwekezaji kwenye miradi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com