MIAKA 60 YA HIFADHI YA TAIFA RUAHA, WAZIRI PINDI AZINDUA UTALII WA PUTO






Na Happiness Shayo


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi,Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi utalii wa puto ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba 7,2024 katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani Iringa.

Akizungumza katika mahojiano maalum ya Kipindi cha Jambo Tanzania ya Shirika la Utangazaji la TBC, Mhe. Chana amesema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii.

"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuionesha dunia vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa tunachangia asilimia 17% na fedha za kigeni takribani dola za kimarekani Bilioni 3.6.

Kuhusu maboresho yaMiundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ruaha Mhe. Chana amefafanua kuwa mpaka sasa kuna barabara ya Iringa- Msembe yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.

Aidha, amesema katika Hifadhi ya Taifa Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Mkoa wa Iringa ambao unaendelea kukarabatiwa.

Amesema ndani ya miaka 3 kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na Serikali inazidi kuboresha maeneo mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post