Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MRADI WA MAJI NGARA KUNUFAISHA MAELFU YA WANANCHI, HISTORIA NYINGINE KUANDIKWA

 

 Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog.

Changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama inatajwa kuwa historia kwa siku za usoni kwa wananchi wa Kijiji cha Katerere Kata ya kanazi Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Ruhoro kukabidhi mradi wenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kwa Mkandarasi unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 16, 2024 ambapo Mkandarasi anatarajiwa kuanza utekelezaji huo ndani ya siku saba ambao utatekelezwa kwa kipindi kisichozidi miezi nane ukiwa na lengo la Kumtua mama ndoo kichwani ambapo mara baada ya kukamilika wanatarajia kuingiza maji kwa kaya 100.


Mradi huo ambao ni neema kwa wananchi hao ni baada ya Serikali kufanya juhudi za muda mrefu za kuchimba visima ambavyo juhudi ziligonga mwamba kwa kukosa maji na hatimaye suluhisho limepatikana.


Ndaisaba amewataka wananchi kutunza mradi huo ili uweze kuwahudumia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kumtaka mkandarasi huyo kufanya kazi nzuri ili kutimiza mkakati wa Serikali ya kuhakikisha mwananchi anapata huduma zote muhimu kwa wakati.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa kufanikisha mpango wa wananchi kupata maji safi.














Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com