NHIF TANGA KUTUMIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA WAO

 


Na Oscar Assenga, TANGA.


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga umesema kwamba watatumia wiki ya huduma kwa wateja kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wanachama wao wanaowahudumia.

Hayo yalibainishwa leo na Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Fredrick Mtango wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba wanatumia siku hiyo pia kuwahudumia wanachama wao ofisini kwao.

Alisema pia wanatarajia kupitia kwenye Hospitali zilizopo Tanga mjini kuonana na wateja wao na kusikiliza changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ili kuweza namna ya kuzipatia ufumbuzi.

“Tunaamini itakuwa wiki njema itakayokuwa na manufaa kwa mfuko na wateja wao kwa ujumla lakini pia nisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kujiunga na mpango wa bima ya afya kuweza kunufaika na huduma za matibabu “Alisema

Awali wakizungumza huduma za mfuko huo baadhi ya wanachama wao akiwemo Noel Mahundi ni Mwalimu Mstaafu kutoka wilaya ya Korogwe alisema huduma za bima ya afya ni nzuri kwa sababu zinawasaidia watu waliokuwa wamestaafu wanapata matibabu wanapokuwa wakiugua.

Alisema huduma zinazotolewa na nzuri kwa sababu zipo ambazo zimeongeka hasa baadhi ya dawa ambazo awali walikuwa hawawezi kuzipata lakini kwa sasa wakienda Hospitalini wanazipata.

Naye kwa upande wake Ailice Barua anashukuru huduma zao ni nzuri na ukienda hospitali unahudumiwa vizuri na upatikanaji wa dawa ni wa uhakika hivyo wasiopokuwa na bima wanapata shida .

Aliwashauri wananchi kuona umuhimu wa kujiunga na mpango wa bima ya afya ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zikiwemo za matibabu bure pindi wanapokuwa wakiugua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post