NHIF YAJIVUNIA WATOAJI HUDUMA ZA AFYA VITUONI

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) unajivunia watoa huduma za Afya kama sehemu ya watu muhimu ya kufikia shabaha ya Bima ya Afya kwa wote na kutimiza malengo ya serikali ya awamu ya sita.


Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Evance Nyangasi ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo walitembelea baadhi ya vituo vinavyotoa huduma za afya vya serikali na binafsi vilivyounganishwa na huduma hiyo.

Amesema wameamua kuwatembelea wanachama wao katika vituo hivyo ili kusikiliza kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata maoni ambayo watakwenda kunifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi wa kina.


"Kama tunavyoelewa lengo na shabaha ya mfuko ni kutoa huduma bora zaidi na kukidhi matarajio zaidi ya wanachama wetu, kituo hiki cha Siha ni moja kati ya vituo 4 vilivyosajiliwa na huduma zetu za NHIF kwa Mkoa huu,

"Tumepeana mrejesho na wahudumu wa hapa lakini pia tumeendelea kupeana elimu juu ya huduma bora kwa mteja, tunaelekea kwenye Bima ya Afya kwa wote ambayo lengo la serikali ni kuona kila Mtanzania anapata huduma ya afya bila tatizo,

"Na ndiyo maana imetafsitiwa kwa vitendo kuhakikisha kwamba vituo vyote vya afya serikalini nchini nzima vinakuwa na huduma toshelezi lakini pia kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuweka miundombinu mizuri ya afya nchini", amesema.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha Siha Polyclinic Dkt. Kasanga Bashir amesema katika maadhimisho hayo wanaendelea kutoa huduma kwa makundi mbalimbali wenye Bima na wasiokuwa nazo.

"Lakini kunfi kubwa la wagonjwa ambao tumewahudumia kwa muda wote ni wateja waliopo chini ya NHIF, niushukuru sana mfuko huu kwa ushirikiano wao wa kutukutanisha na wateja lakini pia kutusimamia katika maziezi mbalimbali kuhakikisha kwamba ushirikiano huu unaenda vizuri" ,amesema.

Dkt. Bashir amebainisha kwamba kufuatia mabadiliko makubwa yaliyofanywa na serikali katika upat8kanaji wa huduma za NHIF kumeleta muitikio mkubwa kwa wananchi jambo ambalo hata wateja wameongezeka kituoni hapo.

"Ikumbukwe kwamba mwaka huu kulikuwa na mtikisiko kidogo wa huduma za NHIF lakini kwa sasa tunashukuru mabadiliko makubwa ambayo yataendelea kufanyika, huduma zinarejea kama kawaida na tunaendelea kupata wateja zaidi wa mfuko", amebainisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post