WATAALAMU NISHATI YA MAFUTA WAWEZESHWE, MUHIMU UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI MAFUTA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SERIKALI imejipanga kuhakikisha kuwa wataalamu katika sekta ya nishati ya mafuta wanapata ujuzi mara kwa mara ili kuendana na kasi ya tekinolojia.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati James Mataragio alipofungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi Taifa (PURA) ambapo taasisi zote ambazo zipo chini ya Wizara hiyo wana fungu la fedha kutoka kwenye mikataba ya uzalishaji na ugawanaji mapato.

Mataragio amesema fedha hizo zinatumika katika kujenga uwezo,, kwahiyo vijana wetu tunawapeleka kwenye mafunzo mafupi kusomea mambo ya gesi ya mafuta katika Mataifa mbalimbali ili kupata ujuzi wa kisasa zaidi.

"Lengo ni kupata wataalamu wabobezi ndani ya nchi, tunaenda kuingia mikataba mikubwa, sasa hivi tunaenda kufanya majadiliano ya kuanzisha mradi mkubwa wa LNG, ni vitu vinavyohitaji ujuzi mkubwa,

"Kwahiyo kuwa na Watanzania waliobobea wataisaidia nchi kuhakikisha kwamba tunapata kazi kubwa zenye mikataba mizuri ambayo itawanufaidha wananchi kwa vizazi vingi vijavyo" amesema Mataragio.

Pia amebainisha kuwa, ni muhimu sana kuwa na wabobezi kwani wataweza kufanya kazi za utafutaji na uchimbaji wa mafuta kama nchi, ambapo kwa sasa hatua kubwa imepigwa kupitia wataalamu waliopata uzoefu.

"Tanzania imepigwa hatua kubwa sana, miaka michache iliyopita hatukuwa na huu uwezo, lakini sasa tumejijenga mpaka kufikia Shirika letu la mafuta linafanya utafutaji lenyewe na tunakwenda mpaka kwenye hatua ambayo tunahitaji mshirika tukishajua ardhini pana kitu,

"Zamani ilikuwa kunakuwa kuna kitalu, unakuita mtu bila kujua ardhini kuna nini, lakini sasa hivi tunajua, kwahiyo inatupa tayari kwamba tunaweka thamani kwenye hilo eneo kabla hujamuita mwekezaji, hivyo hata mkiwa mnajadili eneo mnajua pana kitu" amesema.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post