RC BATILDA AWATAKA WANANCHI KUTUMIA HAKI YAO YA MSINGI KUSHIRIKI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



Na Oscar Assenga, LUSHOTO.

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amewahimiza wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.


Aliyasema hayo wakati akihimitisha zoezi la kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika wilaya za Mkinga, Lushoto na Korogwe ambapo alikutana na wananchi wa makundi mbalimbali.


Alisema kwamba ni muhimu wananchi baada ya kwisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wajipange kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa kupiga kura ikiwemo kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.


“Niwashukuru sana wananchi kwa kushiriki kwenye zoezi hili muhimu la kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura ambapo limehimitishwa Jumapili Octoba 20 hivyo sasa nawaomba tujipange katika kuhakikisha tunatimiza haki ya msingi kuwachagua viongozi.


Aidha alisema hivi sasa ni fursa ya kupiga kura kuwachagua viongozi ambao watakuwa chachu ya kuwaletea maendeleo katika maeneo yenu

“Uchaguzi huu ni muhimu hivyo niwaombe wananchi tuhakikisha tunajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura tuweze kupata haki ya msingi ya kuwachagua viongozi ambao watatuletea maendeleo”Alisema


Aidha alisema ni muhimu wananchi kutumia muda wa lala salama ili kujiandikisha kwenye daftari hilo ili waweze kupata ridhaa ya kuwachagua viongozi ambao watashirikiana na wengine kuwaletea maendeleo.

“Labda niwaambie kwamba viongozi wa Serikali za mitaa ndio msingi wa viongozi wa ngazi za juu hivyo niwaombe wananchi wa maeneo haya kuhakikisha tunajiandikisha lakini tushiriki kwenye zoezi la uchaguzi tuweze kuwachagua viongozi ambao watatuletea maendeleo”Alisema


Awali akizungumza wakati wa zoezi hilo la Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Ikupa Mwasyoge alisema kwamba wilaya hiyo ilikuwa imejiwekea lengo la kuandikisha wananchi 183,575 na hadi sasa wamejiandikisha zaidi ya wananchi 170,000 sawa na asilimia 92.9 na lengo lao ni kufikisha zaidi ya asilimia 100

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post