SAFIRI ZAIDI, LIPA KIDOGO: DUBAI NA JOHANNESBURG KWA AIR TANZANIA


30 Oktoba 2024, Dar es Salaam.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imezindua ofa ya “Safiri Zaidi, Lipa Kidogo” kwa abiria wake wanaosafiri kati ya Zanzibar - Dubai pamoja na Dar es Salaam - Johannesburg.

Uzinduzi huu umehusisha mapokezi ya abiria wa kwanza wa Air Tanzania waliowasili kupitia Kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Zanzibar leo, 30 Oktoba, 2024 wakitokea Dubai.

Kupitia ofa hii, Wateja wa Air Tanzania wanaosafiri kati ya Dubai na Zanzibar au Dar es Salaam na Dubai watafaidika na punguzo la asilimia 20 (20%) la nauli kuanzia tarehe 30 Oktoba 2024.

Safari za moja kwa moja za Dubai - Zanzibar zitafanyika mara tatu kwa wiki kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Uzinduzi wa Kituo hiki kipya cha Dubai – Zanzibar, chenye mvuto mkubwa kwa watalii na shindani kibiashara, kinadhihirisha uwezo wetu katika kuhudumia masoko ya kimataifa ambayo yanatoa fursa nyingi za biashara na utalii kwa wateja. Kutokana na mahitaji makubwa ya wateja, yamechangia ongezeko la miruko ya safari za Dubai hadi kufikia safari za kila siku. Hii inaongeza fursa zaidi za uchaguzi kwa abiria kulingana na mahitaji yao.

Katika kuwajali wateja wake, abiria wa daraja la kawaida wameongezewa idadi ya mabegi hadi kufikia matatu yenye uzito usiozidi kilo 23 kwa kila begi na mabegi manne kwa daraja la biashara, kuanzia leo tarehe 30 Oktoba 2024.

Kwa wateja wake wa Johannesburg Air Tanzania inapenda kuwafahamisha kuwa inarejesha tena safari zake kuanzia tarehe 30 Novemba 2024. Katika kutoa kipaumbele kwa wateja wake wanaosafiri kutoka/kwenda Johannesburg, watanufaika na ofa ya “Safiri Zaidi, Lipa Kidogo” wakiwa kwenye ndege mpya za kisasa B737-9 Max kwa hadhi sawa na safari za kimataifa.

Safari za moja kwa moja za Johannesburg zinamwezesha kila mtu kusafiri nje ya Tanzania huku akifurahia safari yake, ambapo tiketi ya kwenda na kurudi itaanzia $479 na miruko itakuwa mara tano kwa wiki, Jumapili, Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Ratiba hii imezingatia muda rafiki wa kuondoka na kufika ili kuepukana na usumbufu kwa abiria kusubiri kwa muda mrefu anapohitaji kuunganisha safari kwa vituo kama, Mumbai, Dubai, Nairobi, Zanzibar, Kilimanjaro na Mwanza.

Uko tayari kusafiri zaidi kwa kulipa kidogo? Tembelea www.airtanzania.co.tz au piga +255 748 773 900 kukata tiketi yako leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post