SAMIA LOVE ILIVYOKUSANYA, KUONYESHA FURSA KWA VIJANA MBEYA


Swali la umeifanyia nini Tanzania ndilo lililobeba ajenda kuu katika baraza la vijana la Samia Love lililofanyika jijini Mbeya.

Baraza hilo, lililokutanisha mamia ya kundi la vijana limekuwa kielelezo cha tafsiri ya kabla hujaomba onyesha ulichonacho.

Hilo ni kutokana na hotuba na mawasilisho ya vijana mbalimbali katika tukio hilo, walioeleza na kuonyesha mchango wao kwa taifa, badala ya kulalamika.

Walikuwepo waliopoteza mwelekeo wa elimu na baadaye kuibuka vinara wa ubunifu, hivyo kuzalisha maelfu ya ajira, kadhalika wapo waliokuwa kielelezo cha usemi wa vijana ndiyo msingi wa fursa kwa wengine.

Kama unasoma kusubiri fursa kutoka kwa Serikali, baraza hilo limetoa jawabu sahihi la namna kijana anavyopaswa kuenenda ili anufaishwe na mazingira anayoishi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post