TACAIDS YAAGIZWA KUONGEZA KASI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI KATIKA JAMII ZA WAVUVI


Mjumbe wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Afya na maswala ya UKIMWI Mhe. Agnes Marwa akielezea jinsi ambavyo wavuvi walivyo katika hali ya hatari ya kupata Maambukizi ya VVU na umuhimu wa Serikali kuongeza Elimu, huduma za Tiba na matunzo katika jamii ya wavuvi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega akizungumza na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kuhusu namna Wizara yake inavyo tekeleza kuhusu hatau za ujumuishi wa afua za VVU na UKIMWI kwenye sekta ya UVUVI Kilichofanyika tarehe22 Oktoba,2024 Bungeni Dodoma.
Kamati ya Kidumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Mhina wakifuatilia ufafanuzi wa taarifa kuhusu utekelezaji wa hatua za ujumuishi wa Afua za VVU na UKIMWI kwenye sekta ya UVUVI,tarehe 22 Oktoba,2024.
Kamati ya Kidumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Mhina wakifuatilia ufafanuzi wa taarifa kuhusu utekelezaji wa hatua za ujumuishi wa Afua za VVU na UKIMWI kwenye sekta ya UVUVI,tarehe 22 Oktoba,2024.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Afya na Masuala ya UKIMWI Dkt Christine Mzava akizungumzia umuhimu wa kuongeza Afua za UKIMWI katika jamii ya Wavuvi maeneo ya Bahari na Maziwa wakati wa kikao cha kamati hiyo,kilichofanyika Bungeni tarehe 22Oktoba,2024.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bw Samweli Mwashamba akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Waziri kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI jijini Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2024 .


Na Mwandishi Maalum, TACADS

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeagiza Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuongeza kasi ya Utoaji elimu ya kujikinga na VVU, Huduma za Kinga, matibabu na Matunzo miongoni mwa wavuvi katika maziwa na bahari.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Dkt Christina Mzava pamoja na Kamati yake amesema elimu ya kujikinga na VVU miongoni mwa jamii ya wavuvi bado ipo chini hali kadhalika upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI si wa kuridhisha.

Wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakijadili baada ya taarifa ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega kuwasilishwa kwa kamati hiyo kuhusu hatua za ujumuishaji za afua za VVU na UKIMWI kwenye sekta ya Uvuvi wamesema kuwa, elimu ya kujikinga na VVU, pamoja na huduma za kinga,matibabu na matunzo miongoni mwa wavuvi bado zinahitaji kuongeza kasi kwani hali ya maambukizi kwa wavuvi bado ipo juu.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt Christina Mzava alisema TACAIDS bado inakazi kubwa ya kufanya katika sehemu za mialo ili kuokoa jamii za wavuvi kutokana na kuwa na ushamiri wa juu wa VVU kwa asilimia 7 ambayo ni zaidi ya kiwango cha kitaifa.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bw.Samweli Mwashamba akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Mhe Waziri alisema kuwa Wizara na taasisi zake kumi inaendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa afua za VVU,UKIMWI na Magonjwa Sugu yasiyoambukizwa mahala pa kazi kwa mujibu wa waraka No 2 wa Utumishi wa Umma wa Kudhibiti VVU ,UKIMWI na MSY mahala pa kazi katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2014.

Ametaja maeneo yanayotekelezwa na Wizara hiyo kuwa ni pamoja na kujumuisha masuala ya Uvuvi,UKIMWI katika sera ya UVUVI 2015, kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya Utekelezaji wa masuala ya kudhibiti VVU na UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza,kutoa lishe elimu na upimaji wa hiari kwa watumishi pamoja na kaanzisha vituo vya upimaji na ushauri nasaha kwa wavuvi.

Kuunda kamati ya VVU na UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuwa na mratibu ya UKIMWI, usambazaji wa makasha ya kuhifadhi kondomu na kondomu kwenye maeneo ya kazi ya Wizara.

Aidha ametaja sababu zinazopelekea jamii za wavuvi kuwa na maambukizi ya VVU ni pamoja na matumizi hafifu na yasiyosahihi ya kondomu na imani mbovu za kutoamini kondomu zinaweza kutumika na kuleta furaha ya tendo.

 Uelewa mdogo juu ya elimu ya VVU na UKIMWI katika makambi ya wavuvi ambao hupelekea kufanyika kwa ngono zisizosalama pamoja na kutokuwa na tabia ya kupima Afya zao mara kwa mara ilikuweza kuwa ufahamu wa afya zao pamoja na upatikananaji hafifu wa huduma za VVU na UKIMWI katika maeneo ya mialo hasa visiwani.

Sensa za wavuvi ili kuweka mkakati wa namna ya kutoa huduma za upimaji na ushauri nasaha, huduma za VVU na UKIMWI zinazotolewa asilimia 51 katika mialo 1307.

Bw.Samweli Mwashamba amefafanua kuwa jumla ya kondomu 334,872 na makasha 30 ya kuhifadhia kondomu yamesambazwa kwenye Wizara na Taasisi zake katika kipindi cha mwaka 2023/24. 

Lishe na nauli kwa watumishi wa Wizara na Taasisi ambao waliojiweka wazi kuwa wanaishi na VVU katika kipindi cha mwaka 2023/24.

Aidha watumishi 387 walipatiwa elimu ya juu ya VVU na UKIMWI na ushauri nasaha pamoja na kufanyiwa vipimo.













Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post