Na Oscar Assenga, TANGA.
Kubecha aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian na litafanyika Ukumbi wa Samia Business Centre Kange
Alisema kwamba tayari wameshatangaza na kuweka wazi kwenye shule na mitaani ili watoto wajitokeze kushiriki kwenye kongamano hilo litakaloanza saa mbili asubuhi huku akieleza Tanga kuna miradi mingi ambayo Mhe rais Dkt samia suluhuhassaani ameifanyaikwa maslahi mapana ya taifa letu .
“Maandalizi ya Kongamano hili yamekamilika na tunalenga kuwashindanisha vijana,watoto wenye umri wa kati na chini kuwapima uelewa wao wa mambo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Dkt Samia Suluhu ikiwemo katika sekta ya Elimu,Afya,Maji ,Nishati ya Umeme hasa ukizingatia Tanga zamani umeme ulikuwa unakatikakatika sana lakini tokea nimefika sijawahi kuona umeme umekatika”Alisema
Aliseam kwamba yapo mambo mengi mazuri yamefanywa kwa wananchi ikiwemo Miundombinu ya Bandari, Uwanja wa ndege na watu wameanza kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja pamoja na miundombuni barabarani na maeneo mengi ya taa za barabarani.
Hata hivyo alisema pamoja na hayo lakini pia uwepo wa Camera kwa ajili ya kuongeza ulinzi kwenye Jiji la Tanga hivyo wana kila sababu ya kutakiwa kujua vijana na watoto wanafahamu miradi hiyo mikubwa ya kimkakati inayofanyika Serikali nchi ya jemedari Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.
Social Plugin