Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Tanzania imepata tuzo za kimatifa za World Travel kwa mwaka 2024 katika sekta ya Utalii kutokana na juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania.
Tuzo hizo nne zimeendelea kuing’arisha Tanzania Kimatifa katika sekta ya utalii na kuwa Kivutio cha Utalii Afrika (African Leading Tourism Attraction 2024) – Mlima Kilimanjaro na Hifadhi Bora ya Taifa Afrika (Africa’s Leading National Park 2024) – Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea tuzo hizo leo October 22 Dodoma huku akitumia nafasi hiyo Amesema Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi makubwa katika utangazaji utalii kupitia Programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania na kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya utalii nchini.
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Dkt Pindi amesema juhudi zilizofanywa na Dkt. Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa, Mhe. Dkt. Samia kupitia programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania zimeendelea kuing’arisha Tanzania katika sekta ya utalii kwa kupata Tuzo nne za kimataifa
Dkt. Pindi amesema juhudi hizo za Dkt. Samia zimechangia Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kunyakuwa tuzo nne za World Travel Awards kwa mwaka 2024.
Pia tuzo ya Kituo Bora cha Utalii Afrika (African’s Leading Tourism Destination) -Tanzania na Bodi Bora ya Utalii Afrika (African Leading Tourism Board 2024) – Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Dkt. Pindi amesema pia mawakala wa biashara za utalii wa hapa nchini nao wameshinda tuzo katika vipengele mbalimbali kutokana na juhudi zao za kutoa huduma bora katika sekta ya utalii.
Mawakala hao ni Gran Meliá Arusha, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire, Altezza Travel, Satguru Travel Tanzania, Skylink Travel & Tours na Gosheni Safaris.
“Niwapongeze mawakala hawa kwa tuzo walizopata kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika sekta ya utalii.”
Social Plugin