Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji,Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umewapatia mafunzo watia nia ambao tayari wamepitishwa na vyama vyao kwa lengo la kuongeza nafasi za wanawake katika uongozi.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 30,2024 Jijini Dar es Salaam katika semina za jinsia na Maendeleo zinazofanyika kila Jumatano,Afisa TGNP-Mtandao Idara ya mafunzo Anna Sangai amesema katika mafunzo wameyaweka mahususi kwa ajili ya kuwatia moyo kwa kuonesha juhudi za kuongeza nafasi za wanawake katika uongozi.
Sambamba na hayo Bi. Sangai ameeleza kuwa wameandaa mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari,kutoka maeneo mbalimbali kwa dhumuni la kuwafahamisha masuala ya jinsia ili wanapokuwa wanaandika habari zao waandike maudhui yanayohamasisha na sio kukatisha tamaa.
Aidha amesema kupitia mafunzo yao wanayatoa katika semina zao za kila wiki yanawaamsha wanawake kutambua kuwa wananafasi ya kugombea pamoja na kuchagua kiongozi wanayemtaka kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kituo Cha Taarifa na maarifa kata ya Majohe wilaya ya ubungo Tabu Ally ameeleza kuwa changamoto kubwa inayokwamisha wanawake kupitishwa na vyama vyao katika kugombea nafasi za uongozi ni suala la uchumi.
Nae, Mwanaharakati wa Jinsia,Kennedy Anjelita ameshauri watu wote waliojiandikisha kwenda kupiga ili kumpata kiongozi wanaye mtaka bila kujali maamuzi yatakayotolewa baada ya kupiga kura
Social Plugin