Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TPDC MDHAMINI MKUU MBIO ZA MWAL. NYERERE MARATHON, MWANZA


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekuwa Mdhamini Mkuu wa Mbio za Mwl. Nyerere Marathon zilizofanyika leo Jumamosi Oktoba 12, 2024 Igoma Mkoani Mwanza. Mbio hizo zimefanyika zikiwa na lengo la kuenzi falsafa ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Maendeleo na Ustawi wa Taifa letu.

Akiongea katika hafla hiyo Bw. Donald Aponde ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC ameeleza kuwa: 


"TPDC tunajivunia kudhamini mbio hizi kwani Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifanya mambo mengi ikiwemo kuanzishwa Kwa TPDC (1969) ambapo hadi sasa Shirika letu linafanya vizuri kwenye shuguli za utafutaji na uendelezaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia nchini"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com