UJUMBE WA BODI YA PAROLE KUKUTANA MWANZA




Na Mwandishi wetu

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Jeremiah Yoram Katungu, jioni ya leo tarehe 16 Oktoba 2024, amempokea Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Balozi Khamis Kagasheki, pamoja na aliyekuwa Kamishna mstaafu wa Jeshi la Magereza, Juma Malewa. 

Ujumbe wa Bodi hiyo unatarajia kufanya kikao katika Mkoa wa Mwanza kujadili maombi ya wafungwa 131, ili kubaini wenye sifa za kunufaika na parole pamoja na wasiyo na sifa.

Parole ni mchakato wa kumruhusu mfungwa kutoka gerezani na kukamilisha kifungo chake akiwa uraiani, kwa masharti ya kuwa na tabia njema.

Kabla ya mapokezi hayo, CGP Jeremiah Yoram Katungu alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya matunda kadhaa katika eneo la Gereza Kuu Butimba.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post