Na Dotto Kwilasa, Dodoma
UMOJA wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) umelaani vilali kitendo cha wanawake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( BAWACHA) kuchoma kitenge chenye picha ya Rais Samia suluhu Hassan kwa madai kuwa ameshindwa kushughulikia ustawi wa jamii.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda ameeleza hayo leo Oktoba,1,2024 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini hapa ambapo ameeleza kuwa tukio hilo ni lakitoto ,upuuzi huku akiwataka (BAWACHA) kuibua sera zenye mashiko kwa jamiii.
Chatanda ameleza kuwa vitege hivyo vilivyochomwa,UWT walivyogawiwa BAWACHA kama sare kwenye kongamano la siku ya wanawake duniani machi 8 ,2023 na si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kuwa vilitolewa na Rais Samia.
" Kwanza niseme jambo kitenge kilichochomwa ni kitenge kinachoashiria kishindo cha utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi CCM 2020/2025, kitenge hicho kilitengenezwa na UWT Taifa ikiwa ni sare kwa ajili ya kongamano la kumpongeza Rais samia kwa kazi nzuri alitoifanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyofanyika machi 19 2023 , "amesema
Mwenyekiti huyo anafafanua kuwa ,"toleo la kwanza la kitenge hicho lilitolewa machi 13 2023 hivyo ni uongo kusema kuwa Rais Samia ndio aliyewagawia vitenge hivyo kwani siku wanafanya baraza lao kitenge kilikuwa bado hakijatengenezwa bali wanachama wa BAWACHA walinunua kitenge hicho ikiwa ni sare kwaajili ya kongamano kwaajili ya kumpongeza Rais samia na tuliwaalika na waliudhuria kwa wingi, "amefafanua
Aidha amesema Rais samia amefanya mambo makubwa na mazuri kwa Taifa katika nyanja zote hivyo badala ya kuchoma kitenge ni vyema wakatumia muda huo kutangaza fursa zote za kiuchumi ambazo Rais amekuwa akizipigania.
Katika hatua nyingine Chatanda ameipongeza mahakama ya Dodoma chini ya kituo jumuishi cha utoaji haki kwa kutenda haki kwenye kesi ya kubaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti wa yombo Dovya.
Aidha amesema UWT inaendelea kutoa wito kwa jamii kuhakikisha inaendelea kulinda haki na kupinga vitendo vyote vinavyoendelea kwenye jamii ili kuwa na usalama na haki.
Amesema, "Jana washtakiwa walihukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya milioni moja kila mmoja, huu ni ushindi mkubwa dhidi ya mapambano ya unyanyasaji wa kijinsia, " ameeleza