Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Lugoba, Bi. Gloria Kilala akitoa kiapo kwa washiriki wa semina ya daftari la uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa washiriki wa semina katika Ukumbi wa Shule ya sekondari Lugoba
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
MSIMAMIZI msaidizi wa uchaguzi wa Jimbo la Chalinze Bw. Alkanus Kilaji amewasisitiza waandikishaji wa daftari la wapiga kura katika halmashauri ya Chalize kuonyesha taswira ya utumishi wa umma katika zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura.
Bw. Kilaji ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandikishaji wa daftari la wapiga kura wa halmashauri ya Chalinze katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari Lugoba jana.
Bw. Kilaji amesema kwamba waandikishaji lazima wawe na lugha ya staha kwa watakaowahudumia ili kuepuka migogoro katika zoezi zima la uandikishaji.
Msimamizi huyo msaidizi amewataka waandikishaji hao kuwa wavumilivu katika kutekeleza majukumu yao bila kusahau utunzaji wa vifaa vya kuandikisha daftari la wapiga kura.
"Fanyeni kazi kwa viapo, endeleeni kujielimisha juu ya elimu ya uandikishaji na mfanye matumizi sahihi ya simu ili kutokuwakwaza wateja wenu lakini pia viongozi watakao watafuta pindi watakapowahitaji", alisema msimamizi msaidizi huyo.
Naye Mwenyekiti wa semina hiyo Mwalimu Mbaraka Salumu aliwahakikishia watoa mada katika semina hiyo kuwa watakwenda kutekeleza ipasavyo majukumu yao kama jinsi walivyoahidi kwenye viapo vyao.
Zoezi la uandikishaji wa daftari la kupiga kura katika ngazi ya serikali za mitaa litafanyika kuanzia tarehe 11.10.2024 hadi tarehe
Social Plugin