WABUNGE WAMNG'OA MADARAKANI NAIBU WA RAIS KENYA RIGATHI GACHAGUA

YAMETIMIA! Wabunge wa Bunge la Kenya wamemuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya,Rigathi Gachagua, kutokana na mashtaka 11 yaliyokuwa yanamkabili ikiwamo la ufisadi na kuendeleza ukabila akiwa ni kiongozi wa Serikali.

Mashtaka mengine ni pamoja ukiukaji wa Katiba ya Kenya,kutokumheshimu Rais na kwenda kinyume na Sera za Serikali.

Bunge hilo la Kitaifa la Kenya limeidhinisha Gachagua kuondolewa madarakani baada ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Katika kura zilizopigwa kuamua hatma yake, wabunge 281 waliunga mkono hoja ya kumuondoa kiongozi huyo madarakani, huku wabunge 44 wakipiga kura ya kupinga na mbunge mmoja akikataa kupiga kura.

Awali kabla ya kura hizo, kupigwa Naibu Rais hiyo, aliweka matumaini yake kwa Wabunge waliojiandaa kupiga kura kuhusu hoja yake ya kuondolewa madarakani.

Gachagua alisema anaheshimu na anaamini Bunge litafanya uamuzi sahihi.

Naibu huyo, alikuwa akiwahutubia wabunge alipofika mbele ya Bunge kujibu tuhuma zilizowasilishwa kwenye hoja yake ya kuondolewa madarakani.

"Angalia, tafakari, na tumia dhamira yako na ufanye uamuzi yanayofaa," alisema.

"Ninaheshimu sana Bunge na uwezo wake wa kufanya uamuzi sahihi." Kiongozi huyo alitetea hatua yake ya kuzungumzia madai hayo siku moja kabla ya kufika mbele ya Bunge.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post