WADAU SEKTA YA ULINZI BINAFSI WAPIGWA MSASA


Na: Mwandishi wetu, Dar es salaam

Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi, imetoa elimu ya sheria za kazi kwa Wafanyakazi na Waajiri wa sekta za ulinzi Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa amesema kuwa dhumuni la semina hiyo ni kutoa Elimu ya Sheria za Kazi katika Sekta ya Ulinzi nchini ili kuendelea kupunguza changamoto zinazowakabili baadhi ya wafanyakazi katika Sekta hiyo

Aidha, Mkangwa amebainisha baadhi ya malalamiko ambayo yamekuwa yakiripotiwa Idara ya kazi ikiwemo wafanyakazi kuajiriwa bila mikataba, Waajiri kutowasilisha michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuachishwa kazi kiholela bila kuzingatia sheria za kazi.

"Ni matumaini yangu semina hii itakwenda kuondoa changamoto za ukiukwaji wa sheria za kazi ambazo zimekuwa zikiripotiwa ofisini mara kwa mara" amesema.

Awali akizungumza Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Asha Udindo ametoa rai kwa Waajiri wa sekta hizo kujiunga WCF na kuwasilisha michango kwa wakati ili kulinda haki zao dhidi ya majanga yanayoweza kuwapata wafanyakazi wao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.

Naye, Meneja Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Dar es salaam Feruzi Mtika amesema Serikali haitawavumilia waajiri wote wa sekta binafsi ambao wanakata michango ya wafanyakazi wao bila kuiwasilisha katika Mfuko huo.

Kamishna wa Kazi Msaidizi  Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Mwalwisi akiwasilisha mada ya sheria za kazi katika semina ya siku mbili iliyoudhuliwa na wadau wa sekta ya ulinzi binafsi nchini katika ukumbi wa Karemjee hall Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kazi Msaidizi  Vibali vya kazi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Lilian Francis akitoa elimu juu ya mada ya utekelezaji wa sheria katika kipengele cha sheria ya kuratibu ajira kwa wageni
Kamishna wa Kazi Msaidizi Ukaguzi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rehema Moyo akitoa elimu ya utekelezaji wa sheria namna gani ya kusimamia sheria kwa ujumla lakini pia kufanya kaguzi katika maeneo ya kazi kwa minajiri ya kukagua kama wafanyakazi wanapewa mikataba na stahiki mbalimbali za mfanyakazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post