Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WAOMBA JUHUDI ZIFANYIKE KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE VIONGOZI


Imebainika wanawake asilimia 2.1 pekee ndio walijitokeza  Katika kuwania  nafasi za uongozi wa vijiji  jambo ambalo limewaamsha wanaharakati kuona  umuhimu wa kuwekeza juhudi za ziada ili kuondokana na hali hiyo kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo na  usawa wa kijinsia.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 23,2024 na Afisa Idara ya Mafunzo TGNP Anna Sangai   kwenye semina za jinsia zinazofanyika kila Jumatano TGNP-MTANDAO Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Amesema  licha ya kutimia miaka 29 tangu mkutano wa Beijing ulipofanyika takwimu  bado zinaonesha hali sio nzuri hata katika nafasi za uongozi wa vijiji kwani wanawake ni Asilimia 2.1 pekee.

Aidha Sangai  ametoa Rai kwa wanawake waliowania nafasi za uongozi ambao kwa bahati mbaya hawatapita, wanatakiwa kutoa changamoto na vikwazo walivyopitia wakiwa wanagombea nafasi hizo.

Kwa upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia Nelson Munisi ameshauri kuwa mwanamke anapaswa  kutazamwa kwa jicho la kipekee Kama ilivyo katika nafasi za ubunge wa viti maalumu kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia Katika uongozi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com