WANANCHI 250,000 WANATARAJIWA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MULEBA



Mariam Kagenda_Kagera

Jumla ya wananchi 250,000 katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wanatarajia kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaaa na vijiji utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Muleba Isaya Mbenje ametembelea vituo mbalimbali vya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ulioanza leo na kuzunguma na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Wilaya ya Muleba Ina kata 43 na vijiji 166 huku vituo vilivyotengwa kwa ajili ya zoezi la uandikishaji vikiwa ni 802.

Amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yamekamilika na vituo vyote vimefunguliwa huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Muleba Dr Abel Nyamahanga amesema kuwa anatambua Wilaya ya Muleba imezungukwa na visiwa vingi hivyo ametoa wito kwa ambao sio wakazi wasishiriki zoezi Hilo kwani zoezi Hilo linawahusu wakazi wenyewe wa eneo Hilo kwenye Vitongoji na vijiji husika.

"Tunawingi wa visiwan na maeneo yetu kunawafanyabishara wengi wanakuja katika visiwa vyetu , tunahamasisha shughuli ziendelee lakini kama sio mtanzania au mkazi usidhubutu kujiandikisha katika Daftari au kushiriki uchaguzi huo.
Jilala chobo mwananchi wa kitongoji Bugombe Wilaya ya Muleba amesema ili wananchi wawapate viongozi wanaotaka wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kwani maamuzi pekee ya kumpata kiongozi wa kweli ni kujiandikisha ili usubiri kupiga kura Yako.

"Wanachi wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kiongozi afai lakini hawajui kuwa namna pekee ya kumpata kiongozi Bora ni kujiandikisha na kujitokeza kumpigia kura hivyo nawashauri wananchi wenzangu wajitokeze kujiandikisha "alisema Chobo.

Wakala wa Chama Cha Siasa Hassan Ayub akiwa katika kituo Cha uandikishaji cha Kijiji Magata alipongeza utaratibu uliowekwa na serikali katika maswala ya uandikishaji kwa kuhakikisha Kila mwenye haki ya kujiandikisha anapata Fursa ya kujiandikisha bila kubuguziwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post