Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA Temeke imetekeleza zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja wapya 38 kutoka maeneo ya Keko, Kerezange, Mtoni na Tandika
Aidha kupitia zoezi hilo elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji na njia rasmi za malipo ya huduma za maji pamoja na mawasiliano ya Mamlaka na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA imetolewa kwa wateja hao.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0737-730523 (DAWASA Temeke).
Social Plugin