Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe.Dkt. Isaac Njenga na Ujumbe wake katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam Oktoba 8, 2024.
Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza ushirikiano wa Kibiashara hasa katika Biashara za mipakani, Biashara za mazao ya Kilimo pamoja na kubadilishana Elimu na Teknolojia na kushirikiana nguvukazi viwandani.
Social Plugin